Serikali kuondoa marufuku ya safari za usiku baada ya marufuku hiyo kubatilishwa na mahakama

Posted by Jenniffer Sheldon on Saturday, September 21, 2024

- Serikali imo katika harakati ya kuondoa marufuku dhidi ya safari za usiku kwa magari ya umma kufuatia uamuzi wa mahakama

- Akilihutubia bunge siku ya Jumatano, Januari 17, katibu mkuu wa usafiri, Paul Mwangi alisema kuwa serikali inatarajia kurejesha safari za usiku kwa magari ya umma hivi karibuni

Wakenya ambao hupendelea kusafiri usiku badala ya mchana watapata afueni baada ya serikali kutangaza kuwa na mpango wa kufutilia mbali marufuku iliyoweka kwa magari ya umma kusafiri usiku.

Habari Nyingine: Mambo muhimu yasiyofunzwa katika Vyuo Vikuu

Akiongea katika Bunge siku ya Jumatano, Januari 17, katibu mkuu katika wizara ya usafiri, Paul Mwangi alifichua kuwa serikali inapanga kurejesha safari za usiku kwa magari ya umma ya masafa marefu.

Habari Nyingine: Prezzo akutana na bintiye baada miaka, furaha yake haifichiki(video)

Marufuku hiyo iliwekwa na mamlaka ya NTSA wiki mbili zilizopita kufuatia ongezeko la ajali barabarani hasa mwezi wa Desemba 2017.

Hatua ya kuiondoa marufuku hiyo imejiri baada ya mazungumzo ya kina kati ya washika dau kwenye idara hiyo ya usafiri wa umma.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka Read more:

Haya yanajiri pia wiki moja tu baada ya mahakama moja Nakuru kubatilisha marufuku hiyo ya serikali. Kulingana na mahakama hiyo, hakuna sheria yoyote iliyounga mkono marufuku hiyo ya serikali dhidi ya safari za usiku kwa magari ya abiria ya masafa marefu.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4B0gpFmqp6qmaCurbWMpKyoppSkrm65wKusn62bqnq6rYysmJ%2BZop56u62Mrqqio6Vir6Ktw5pkspldoq6zwcWuoq5lmJ7GsHnKrpmarJmhtrS01ppkp5ldoq6prcqapJpmmKm6rQ%3D%3D