Kakamega: Ndugu wawili wakamatwa kwa kumuua mama yao

Posted by Martina Birk on Monday, September 30, 2024

- Ndugu wawili kaunti ya Kakamega wamedaiwa kumuua mama yao mwenye umri wa miaka 65

- Kwa sasa wamezuiliwa na maafisa wa polisi uchunguzi dhidi yao ukiendelea, hata hivyo haijabainika kilichosababisha wawili hao kutekeleza kitendo hicho

- Mwili wa mwendazake ambaye pia alikuwa akihudumu kama mhubiri umehifadhiwa katika mochari ya hospitali ya Kakamega

Ndugu wawili kutoka kijiji cha Shisele eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega wametiwa mbaroni baada ya kumuua mama ya kinyama.

Habari Nyingine: Maisha yangu yamo hatarini, Seneta Irungu Kang'ata adai

Habari Nyingine: Uchaguzi Mkuu Uganda: Bobi Wine na mkewe Barbie warauka kupiga kura

Mwili wa mama Benedina Nabwangu ulipatikana Jumatano, Januari 13 mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ukiwa kwenye dimbwi la damu.

Benson Muhanji ambaye hulinda mifugo nyumbani kwa marehemu alisema alipata mwili wake ukiwa na majeraha ya kisu kwenye kichwa chake.

Kwa mujibu wa taarifa za Nation, mshukiwa mmoja ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mwingine ni kaka wa kambo na walikuwa wakiishi na mama huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 65.

Baada ya kutekeleza kitendo hicho cha unyama wawili hao wanasemekana kutoroka nyumbani bila kumwarifu yeyote kuhusiana na kifo cha mama yao.

Habari Nyingine: Rais Museveni achapisha kibonzo cha video yake akidensi Jerusalema kupiga kampeni za mwisho

Mwanafunzi huyo wa chuo kikuu alikamatwa akiwa safarini kuelekea jijini Nairobi, akifanyiwa uchunguzi alisema kwamba alitoroka nyumbani baada ya watu wasiojulikana kuwavamia.

Hata hivyo, maafisa wa polisi hawakuridhishwa na madai hayo, walimuuliza sababu ya yeye kutopiga ripoti kwa polisi.

Kamanda mkuu wa polisi kaunti ya Kakamega alisema uchunguzi zaidi unafanywa kubaini chanzo cha mauaji.

Mwili wa mwendazake ambaye pia alikuwa akihudumu kama mhubiri umehifadhiwa katika mochari ya hospitali ya Kakamega.

Habari Nyingine: Regina Daniels amzawadi mamake gari la kifahari siku yake ya kuzaliwa

Visa vya watoto kuwauwa wazazi wao vimekithiri nchini, wiki jana mvulana wa miaka 22 kutoka kaunti ya Kiambu aliwauwa wazazi wake, ndugu yake, binamu yake na mlinzi wao.

Lawrence Warunge aliambia mahakama kwamba alitekeleza mauaji hao kwa sababu wazazi wake hawakuwa wanamjali wala kumpenda.

Mshukiwa pia alidai wazazi wake walikuwa wakishiriki ushirikina na hivyo walistahili kufa.

Kwa sasa Lawrence amezuiliwa kwa siku 14 pamoja na mpenzi wake ambaye anadaiwa kununua kisu kilichotumika kuwauwa wazazi wake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjboZ5gphmopqjkaKyqK2Mp5uun6VixKLDyKWgZq%2BRoK6urdOwmGajp5Z6rMHMrqyaZZ2WuqJ52JqmZ6Ckork%3D